Rais wa Kenya aahidi kukomesha utekaji nyara
28 Desemba 2024Matangazo
Akizungumza na umati wa watu jana Ijumaa akiwa mjini Homa Bay magharibi mwa Kenya, Ruto aliahidi kukomesha utekaji nyara huo lakini pia akawaambia wazazi "kuwajibikia" kwa watoto wao. Vikosi vya usalama katika taifa hilo la Afrika Mashariki vimeshutumiwa kwa kuwashikilia watu kadhaa kinyume cha sheria tangu maandamano yaliyoongozwa na vijana dhidi ya serikali mwezi Juni na Julai. Matukio ya hivi karibuni yamehusisha hasa vijana ambao wamemkashifu Ruto mtandaoni, huku mashirika ya kutetea haki ya binadamu yakikanusha madai ya polisi kutohusika na kutaka hatua zichukuliwe.