SiasaAsia
Rais wa Korea Kusini alikiuka pakubwa katiba na sheria
4 Desemba 2024Matangazo
Muswada huo uliowasilishwa na wabunge wa upinzani umeoenyesha Yoon alikiuka pakubwa sheria na katiba na kuongeza kuwa hatua hiyo haikuchochewa na mashaka ya kiusalama, bali alilenga kuepuka uchunguzi wa madai ya uhalifu unaomuhusisha Rais Yoon. Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amezungumzia hatua hiyo, akisema inatia wasiwasi mkubwa. Katika hatua nyingine, Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini Kim Yong Hyun amewasilishwa barua ya kujiuzulu kufuatia mzozo huo.