Hatimae rais Joe Biden wa Marekani anakwenda Angola
1 Desemba 2024Rais anayeondoka madarakani nchini Marekani,Joe Biden anaanza ziara yake nchini Angola kuanzia Jumatatu, akitimiza ahadi muhimu aliyoitowa 2022 ya kuimarisha mahusiano na bara la Afrika kwa kuitembelea nchi hiyo.
Biden atakaa mjini Luanda, mji mkuu wa Angola, kuanzia Jumatatu hadi Jumatano ,akiwa rais wa kwanza wa Marekani kuitembelea nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika yenye utajiri wa mafuta,tangu ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Wareno mwaka 1975.
Akiwa Angola anataka pia kuimarisha uwepo wa Marekani katika bara hilo katika kiwingu cha kuongezeka kwa uwekezaji unaofanywa na China.
Rais Biden ambaye kwa sasa hana maamuzi makubwa, wakati anajiandaa kumkabidhi madaraka Donald Trump Januari 20, alipanga mwazoni kufanya ziara yake hiyo mwezi Oktoba lakini ilisogezwa mbele kutokana na kimbunga Milton kilichopiga katika jimbo la Florida.
Hata hivyo afisa mmoja mwandamizi katika serikali ya Marekani amesema ziara hii ya Biden bado haijachelewa.Soma pia: Blinken kuzuru Afrika wakati mizozo ikiendelea kutatiza sera ya kigeni ya Marekani
Yatakayojadiliwa Luanda
Rais Biden atajadili kuhusu masuala mbali mbali ya uwekezaji akiwa mjini Luanda,ikiwemo mradi wa mkubwa wa reli wa Lobito,ambao unahusisha ujenzi wa reli hiyo inayounganisha bandari ya Agola ya Lobito hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,ikiunganisha hadi Zambia.
Mradi huo wa ujenzi wa kilomita 1,300 umegharimiwa na Marekanii pamoja na Umoja wa Ulaya na umetajwa na rais Biden kama ndio uwekezaji mkubwa wa reli barani Afrika kuwahi kufanyika.Soma pia: Angola, DRC zalenga ukarabati wa reli muhimu kukidhi kiu ya madini duniani
Mradi huo wa kimkakati unaiunganisha bandari na migodi ya Kobalti na shaba,madini muhimu katika utengenezaji wa betri za simu za mkononi za kisasa pamoja na utenezaji wa bidhaa nyingine za kiteknolojia.
Atakuwa na mkutano na rais Joao Lourenco wa Angola na kutowa hotuba kuhusu masuala ya afya ya umma,kilimo,ushirikiano wa kijeshi na uhifadhi wa urithi wa kitamaduni.
Lakini pia mashirika ya kutetea haki za binadamu yametowa mwito kwa rais huyo wa Marekani kulizungumzia suala la rekodi mbaya ya Angola ya haki za binadamu katika ziara yake hii.
Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni za Amnesty International,Polisi wa Angola wamehusika katika mauaji ya takriban waandamanaji 17 ikiwemo wa umri mdogo,katika harakati zao za kuwaandama wapinzani