Rais wa Mauritania ataka nguvu ya pamoja kuushinda ugaidi
23 Juni 2024Hayo kayasema katika mahojiano yake na AFP kabla ya uchaguzi wa rais wa Juni 29.Amenukuliwa akisema "Kanda lazima itengeneze nia ya pamoja ya kisiasa ili kuweza kupambana na ukosefu wa usalama." Aidha aliongeza kwa kusema hali ya usalama katika kanda hiyo sio nzuri hata kidogo na imeeendelea kuwa mbaya zaidi.
Mkuu huyo wa zamani wa jeshi na waziri wa ulinzi mwenye umri wa miaka 67 anatarajiwa kuhudumu kwa muhula wa pili kama mkuu wa nchi yenye watu milioni 4.5 ambayo iko kimkakati kati ya kaskazini na kusini mwa jangwa la Sahara.
Katika miaka ya hivi karibuni majeshi yalijitwalia mamlaka kwa nguvu katika nchi za Mali, Burkina Faso na Niger na hivyo kuzidisha hali ya sintofahamu katika eneo hilo. Taifa kubwa la jangwa la Rais Ghazouni lina pakana na Mali kwa mpaka wa zaidi ya kilomita 2,000.