1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Rais wa mpito wa Korea Kusini awaondoa hofu washirika wake

15 Desemba 2024

Rais wa mpito nchini Korea Kusini Han Duck-soo amewatoa hofu washirika wa taifa hilo na kujaribu kuyatuliza masoko ya fedha siku moja baada ya Rais Yoon Suk Yeol kupigiwa kura ya kuondolewa madarakani.

https://p.dw.com/p/4oAC4
Rais wa mpito Han Duck-soo
Rais wa mpito nchini Korea Kusini Han Duck-soo, ameahidi utulivu wa masoko ya fedha katika kipindi cha mpitoPicha: Yonhap/picture alliance

Han alizungumza na Rais Joe Biden wa Marekani kwa njia ya simu jana Jumamosi na kumwambia Korea Kusini itaendeleza sera zake za kiusalama na za nje bila ya usumbufu wowote na kuhakikisha ushirika na Marekani unadumishwa kwa uthabiti.

Han amechukua nafasi hiyo kupitia amri ya katiba, baada ya jaribio lililoshindwa la rais Yoon Suk Yeol kutangaza sheria ya kijeshi..

Chama kikuu cha upinzani kimetangaza kutoendelea na mchakato wa kumshtaki Han kwa ushiriki wake katika uamuzi wa Yoon wa kutangaza sheria ya kijeshi Disemba 3, ili kutuliza uchumi na uongozi nchini humo.