1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Taiwan akutana na spika wa bunge la Marekani

6 Aprili 2023

Spika wa Baraza la Wawakilishi nchini Marekani Kevin McCarthy amesema yeye pamoja na kundi la wabunge wa vyama vya Republican na Democratic wamefanya mkutano muhimu na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen hapo jana.

https://p.dw.com/p/4Pkyl
Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen na Spika wa bunge la Marekani Kevin McCarthy
Spika wa bunge la Marekani Kevin McCarthy alipokutana na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wenPicha: Ringo H.W. Chiu/AP Photo/picture alliance

Spika wa Baraza la Wawakilishi nchini Marekani Kevin McCarthy amesema yeye pamoja na kundi la wabunge wa vyama vya Republican na Democratic wamefanya mkutano muhimu na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wenhapo jana. McCarthy amesema Marekani inastahili kuendelea kuiuzia Taiwan silaha na kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi kwa biashara na teknolojia.

Spika huyo ameongeza kwamba Marekani itaendelea kuiunga mkono Taiwan. Kwa mkutano huo wa jana, McCarthy sasa amekuwa kiongozi wa ngazi ya juu wa Marekani kukutana na kiongozi wa Taiwan nchini Marekani tangu mwaka 1979.China yamuonya Spika wa Marekani dhidi ya kukutana na Rais wa Taiwan Haya yamefanyika licha ya kitisho cha China iliyodai kwamba italipiza kisasi kwa mkutano huo. China inaichukulia Taiwan yenye utawala wa ndani, kuwa chini ya himaya yake.