1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Tunisia awalaumu wafungwa kwa misukosuko ya nchi

15 Februari 2023

Rais wa Tunisia Kais Saed amewatuhumu baadhi ya watu wanaoshikiliwa kufuatia wimbi la karibuni la kamatakamata, akiwahusisha na ongezeko la gharama na uhaba wa chakula nchini humo

https://p.dw.com/p/4NV14
Tunesien I Protest gegen Kais Saed in Tunis
Picha: Yassine Mahjoub/NurPhoto/picture alliance

Rais Saed aidha ameapa kuendela na hatua za kile alichokiita "kuisafisha nchi" katika matamshi yake rasmi na ya kwanza kuyatoa kuhusiana na kamatakamata hiyo, wakati alipokutana na waziri wa biashara wa Tunisia.

Wakosoaji wa serikali wakamatwa Tunisia

Kwenye video iliyosambaa mitandaoni, Saied amesema, kamatakamata hiyo ya karibuni imeonyesha wahalifu wengi waliojihusisha na kula njama dhidi ya usalama wa ndani na nje ya taifa hilo ndio wanaohusika na mizozo ya usambazaji wa vyakula na mfumuko wa bei, ingawa hakufafanua kwa kina namna wanavyohusika.

Mwanaharakati wa Tunisia Khayam Turki akamatwa na polisi

Tangu siku ya Jumamosi, polisi imewakatama wapinzani dhidi ya Saied ikiwa ni pamoja na wanasiasa na wafanyabiashara maarufu pamoja na mmiliki ya shirika pekee kubwa la binafsi la habari nchini humo.