1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Rais Zelensky kuzungumza na Waziri mkuu wa Ireland

13 Julai 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky hii leo anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ireland Simons Harris katika uwanja wa ndege wa Shannon ulioko magharibi mwa Ireland.

https://p.dw.com/p/4iF5D
Schweiz Gipfeltreffen zum Frieden in der Ukraine
Rais wa ukraine Volodymyr Zelensky alipokuwa kwenye mkutano wa kilele wa Amani nchini Ukraine nchini Uswisi Juni 15, 2024Picha: EPA/MICHAEL BUHOLZER

Haya yatakuwa ni mazungumzo ya kwanza baina ya mataifa hayo mawili kufanyika huko Ireland na yatajikita katika vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Kwenye mazungumzo hayo pia, Harris anatarajiwa kutoa salamu za pole kwa familia za watu waliopoteza jamaa zao kutokana na vita, na hususan katika shambulizi la bomu kwenye hospitali kubwa ya watoto mapema wiki hii.

Harris aliyeingia madarakani mwezi Aprili anataraji kuzungumzia msaada zaidi kwa maelfu ya watoto wa Ukraine waliopelekwa kinguvu nchini Urusi na Belarus tangu vita hivyo vilipozuka na kuingizwa kwenye mfumo wa elimu wa Urusi.