Durtete aetea vita alivyovianzisha dhidi ya dawa za kulevya
28 Oktoba 2024Kiongozi huyo wa zamani ametowa ushahidi leo mbele ya baraza la seneti linalochunguza matukio yaliyofanyika chini ya utawala wake ya kuwaandama wale waliotajwa kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.
Polisi ilisema kampeni hiyo ilisababisha vifo vya watu 6,000 ingawa mashirika ya kutetea haki za binadamu yanakadiria kwamba maelfu ya watu na hasa wanaume masikini waliuwawa na maafisa wa polisi na makundi ya mgambo na mara nyingi bila ya ushahidi wa kuhusika kwao na dawa za kulevya.
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC inachunguza madai kwamba mauaji hayo yaliyofanyika Ufilipino yalifikia viwango vya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Katika taarifa yake ya kujitetea nchini mwake, Durtete mwenye umri wa miaka 79 amelitaka baraza la seneti kutohoji sera zake na hatoomba radhi kwa sababu alifanya alichobidi kufanya kuondowa mihadarati.