1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Yoon wa Korea ashindwa kufika kwa mahojiano ya ufisadi

18 Desemba 2024

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol ameshindwa kufika mbele ya shirika la kupambana na ufisadi nchini humo baada ya kuitwa kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu jaribio lake la kutangaza sheria ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4oI64
Südkorea, Seoul | Präsident Yoon Suk-yeol spricht zur Nation nach Aufhebung des Kriegsrechts
Picha: South Korean Presidential Office/Getty Images

Wachunguzi kutoka shirika hilo la kupambana na ufisadi CIO walimuita Yoon katika ofisi yao mapema leo ili kuhojiwa kuhusu mashtaka ya uasi na matumizi mabaya ya mamlaka.

Mawakili wa Yoon wamesema kiongozi huyo hakufanya uasi na wameapa kupinga mashtaka hayo mahakamani.

Yoon aliondolewa madarakani na bunge mwishoni mwa wiki baada ya kutangaza sheria ya kijeshi mnamo Disemba 3, hatua iliyosababisha mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini humo.