Rais Zelensky ataka Marekani iipigie chapuo kuingia NATO
1 Desemba 2024Matangazo
Zelensky amesema katika mkutano wake na waandishi habari mjini Kiev, kwamba hatua yoyote ya kuialika nchi yake kujiunga na NATO inapaswa kuhusisha maeneo yote ya nchi hiyo isipokwa yale yanayokaliwa yanayokabiliwa na vita vinavyoendelea. Kwa mujibu wa kiongozi huyo,Ukraine inahitaji kuwemo ndani ya NATO ili iendelee kuwepo,wakati ikipambambana na Urusi. Ametowa mwito wa kupatiwa silaha,na hakikisho la kiusalama kabla ya kukaa kwenye meza ya mazungumzo na Urusi.