1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Ramaphosa apongeza ahadi ya China kwa Afrika

5 Septemba 2024

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema ahadi ya kiongozi wa China Xi Jinping, ya kufadhili kiasi cha dola bilioni 50 kwa bara la Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo kuwa ya faida kubwa kwa bara hilo.

https://p.dw.com/p/4kK6o
Mkutano wa kilele wa China na Afrika
Jumla ya wawakilishi 53 wa Afrika wakiwemo marais na wakuu wa nchi wanahudhuria mkutano wa kilele ambao umeandaliwa na China mjini BeijingPicha: Andy Wong/AP/picture alliance

Ramaphosa amesema ana mtazamo chanya kwa kiasi hicho cha fedha kilichotangazwa rais Xi hii leo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing wakati wa ziara ya kiserikali iliyojumuisha kuhudhuria kongamano la China na Afrika.  

Rais huyo wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema haamini kwamba uwekezaji wa China barani Afrika una nia ya kulisukuma bara hilo katika mtego wa madeni bali badala yake anaiona kuwa ni sehemu ya uhusiano wenye manufaa kwa pande zote.

Wajumbe kutoka kwenye zaidi ya mataifa 50 ya Afrika wamekusanyika mjini Beijing wiki hii kuhudhuria kongamano hilo kati ya China na Afrika.