1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti: Vichanga nusu milioni wafa kwa uchafuzi wa hewa 2019

21 Oktoba 2020

Utafiti mpya unaonesha maelfu ya watoto wachanga, na hasa India na mataifa ya Afrika katika eneo la Kusini mwa Sahara kwa mwaka 2019 wamekufa kutokana na uchafuzi wa hewa. Kiini cha uchafuzi huo ni moshi wenye sumu.

https://p.dw.com/p/3kEQh
Indien | Neugeborene im Krankenhaus in Sangareddy
Picha: Getty Images/AFP/M. Sharma

Idadi watoto wachanga wanaokadiriwa kufikia 476,000 kote ulimwenguni walifariki kutokana na athari mbaya za zinazotajwa kutokana na uchafuzi chafuzi wa hewa katika kipindi cha 2019. Utafiti huo ambao unajikita katika utambuzi wa mazingira ya dunia, ambao umetolewa hivi karibuni, unasema theluthi mbili ya vifo hivyo vilivyotajwa, vinahusiana na kwa mafuta yenye kiwango duni yanayotumika kama nishati ya upishi wa majumbani.

Rekodi za utafiti huo mpya zinaonesha watoto wachanga wapatao 236,000 wanakadriwa kufa kwa sababu zinazohusiana na uchafuzi wa hewa barani Afrika katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara na zaidi ya wengine 116,000 nchini India. Pakistan pia inatajwa kuwa na zaidi ya vifo vya watoto wachanga 50,000 kutokana na kadhia hiyo ya uchafuzi wa hewa.

Slum in Freetown in Sierra Leone
Uchafuzi wa hewa umetajwa kuchangia vifo vya karibu vichanga nusu milioni katika maeneo mbalimbali ya dunia.Picha: picture-alliance/dpa/T. Ridley

Kulingana na utafiti huo, kina mama wanapokumbwa na uchafuzi mkubwa wa hewa, inaweza kuleta hatari kubwa ya watoto wao, ambapo wanaweza kuzaliwa wakiwa na uzito mdogo au kuzaliwa kabla ya wakati kwa maana ya watoto njiti.

Hali hiyo kimsingi inaweza kusababisha au kuongeza hatari ya watoto kufa katika mwezi wa mwanzo wa maisha yao, lakini pia kuwa na athari mbaya kwa afya yao kwa maisha yote endapo walinusurika utotoni.

Uchafuzi wa mazingira watajwa kuchukuwa nafasi kubwa

Ingawa utafiti huo ulibaini kwamba asilimia 64 ya vifo vilitokana na uchafuzi wa hewa majumbani, lakini uchafuzi wa mazingira kwa ujumla wake pia ulichukua nafasi kubwa, haswa Kusini mwa Asia, ambapo asilimia 50, ya vifo vya watoto wachanga vilihusishwa na athari ya uchafuzi wa hewa kutoka nje ya nyumba zao. Yaani ikujumisha mazingira yanayowazunguka.

Wohnsiedlung mit dem Kraftwerk Gersteinwerk
Kiwanda cha kufua umeme kwa kutumia nishati ya makaa ya mawe.Picha: picture-alliance/S. Ziese

Kwa mujibu wa utafiti huo, uchafuzi wa hali ya hewa kwa ujumla ulisababisha vifo milioni 6.7 ulimwenguni kote katika kipindi hicho cha mwaka 2019. Kwa hivyo kiwango hicho kinaufanya uchafuzi wa hewa kuwa sababu ya nne inayoongoza kwa vifo vya mapema kabla nyingine ambazo ni shinikizo la damu, matumizi ya tumbaku na lishe duni.

Waandishi wa utafiti huu mpya kuhusu hali ya hewa duniani wamegundua kwamba kumekua na hatua kidogo zilizopigwa katika kukabilana na tatizo hilo au kwa maneno mengine hakuna kabisa kilichofanyika katika jitihada za kupunguza uchafuzi wa hewa katika maeneo mengi ya ulimwengu, licha ya kuwepo ushahidi unaoongezeka katika kuonyesha athari zake kwa afya ya binadamu.

Miongoni mwa mambo mengine, wamesema kwamba kupatwa na athari zitokanazo na uchafuzi wa hewa kwa kipindi fulani kunaweza kusababisha sio tu hali mbaya ya kiafya, bali pia kuwafanya watu wawe katika hatari zaidi ya kupatwa na uogonjwa wa COVID-19 katikati ya janga la sasa linaloendelea kuisumbua dunia.

Chanzo: Mashirika