1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya 2009 ya Shirika la Amnesty International.

28 Mei 2009

Msukosuko wa kiuchumi duniani, umegueka sasa kuwa silaha kubwa ya ugandamizaji wa haki za watu kote duniani. Sura hii imetolewa na shirika la Amnesty International katika ripoti yake ya mwaka wa 2009.

https://p.dw.com/p/HzD7
Ripoti ya 2009 ya Amnesty International.Picha: picture alliance/dpa

Shirika hilo hasa limesema mataifa maskini na hasa nchi za Afrika zimepata pigo kubwa. Rekodi ya haki za kibindamu katika nchi nyingi Afrika ni ya kukata tamaa na sasa mgogoro huu wa kiuchumi umezidisha zaidi matatizo ya haki za kibinadamu.



Entführung Ärzte ohne Grenzen Mitarbeiter in Darfur
Watoto Afrika wakipanga foleni kupata chakula.Picha: AP

Ripoti hii inasema swala la kuanguka kwa uchumi duniani imezua matatizo mapya Afrika. Mbali na zile taabu za tangu jadi kama walio wachache kutengwa- kufurushwa kwa maskini katika maskani zao katika mitaa ya mabanda na swala la wakimbizi, shida mpya zimejitokeza. Kulingana na Erwin van der Borght mkurugenzi wa Amnesty Intenational anayehusika na maswala ya Afrika - matatizo mapya yaliyojitokeza ni pale waliposhuhudia raia wa mataifa kadhaa Afrika wakijitokeza na kuandamana kulalamikia hali ya juu ya maisha. Bei za juu za vyakula na mahitaji muhimu.


Na cha kusikitisha anasema Van der Borght ni pale serikali kadhaa zilipotumia nguvu kupitia kiasi kukabiliana na maandamano kama haya.Mfano Cameroon watu 100 waliuawa pale polisi walipotumia nguvu .


Shirika la Amnesty pia lilitaja katika ripoti yake mwaka huu- kwamba licha ya haki za watu kugandamizwa na hali hii ya kiuchumi kuna maswala mengine ya haki za kibinadamu hayakupewa umuhimu kama inavyotakikana . Maswala haya kulingana na ripoti hii ni dhulma dhidi ya wanawake na matatizo wanayokumbana nao watu wanaoishi katika maeneo yenye mizozo kama jimbo la Darfur nchini Sudan na Somalia.


Serikali hasa za Afrika zipo mbioni kunyoosha masoko yake. Lakini masoko na taasisi za kiuchumi hazitoshughulikia matatizo ya kugandamizwa kwa haki za kibinadamu- Ripoti hiyo iliendelea kusema. Shirika hili la Amnesty International linasema mgogoro huu wa kiuchumi ulioangusha masoko kote ulimwenguni ndio pigo la pili kubwa kwa haki za kibinadamu baada ya yale mashambulizi ya septemba 11 nchini Marekani- Pale haki za kibinadamu zilitupiliwa mbali.


Somalia Soldat aus Äthopien in Somalia
Hali nchini Somalia- vita vimewaua wengi na kuwaacha wengi bila makaazi.Picha: AP

Benki ya dunia inazungumzia kwamba watu milioni 53 watasukumwa zaidi katika limbi la umaskini- na hasa Afrika . Mwaka jana watu milioni 150 pia wengi ikiwa ni Afrika waliathirika na ukosefu au uhaba wa chakula- na hii inaashiria kwamba hatua nyingi zilizopigwa kukabiliana na uhaba wa chakula zimepigwa kumbo na mgogoro huu wa kiuchumi.


Van der Borght ambaye hasa anashughulikia Afrika anasema nchi zilizoendelea zinapokabiliana na kuyanyoosha masoko yao na taasisi zao za kiuchumi zisiisahau Afrika, waendelee kutoa misaada. Lakini pia anasema viongozi wa Afrika pia wana jukumu kubwa la kupigana na ufisadi.


Shirika la Amnesty International sasa limezindua kampeini ya kupigania hadhi ya utu na kuhakikisha haki hizi hazivunjwi au haziko hatarini kutokana na mgogoro huu wa kiuchumi.


Mwandishi: Munira Muhammad_/ IPS

Mhariri: Abdul-Rahman