1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUreno

Ronaldo afunga bao la 901 katika ushindi dhidi ya Scotland

9 Septemba 2024

Cristiano Ronaldo alitokea benchi na kufunga bao lake la 901 na kuisaidia timu yake ya taifa ya Ureno kupata ushindi muhimu wa 2-1 dhidi ya Scotland katika mchezo wa ligi ya mataifa ya Ulaya UEFA Nations League.

https://p.dw.com/p/4kQwM
Portugal | Fußballspiel der UEFA Nations League zwischen Portugal und Kroatien
Cristiano Ronaldo akisherehekea baada ya kufunga bao dhidi ya Croatia katika uwanja wa Luz, mjini Lisbon.Picha: Armando Franca/AP Photo/picture alliance

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 aliweka rekodi mapema wiki hii kwa kufunga bao lake la 900 akiwa na klabu na timu ya taifa.

Hadi sasa, Ronaldo amefunga mabao 901 katika mechi 1238, ikiwa ni wastani wa mabao 0.73 kwa kila mchezo.

Ronaldo ameweka wazi nia ya kufikisha mabao 1000 licha ya kuwa mwisho mwisho wa taaluma yake ya soka.

Soma pia: Ronaldo: Bado sijafikiria kustaafu soka

Kocha wa timu ya taifa ya Ureno Roberto Martinez amesema, "Sidhani kama kuna mtu yeyote mwenye mashaka juu ya uwezo wa Ronaldo. Ni kitu cha ajabu anachokifanya kwenye soka. Lakini kwa upande wetu, lengo ni moja. Cristiano anaweza kuisaidia timu ya taifa, na kwangu mimi sio suala la kufunga mabao tu. Anatoa pasi zinazosaidia kupatikana kwa mabao. Iwapo atafanikiwa kutoa pasi 100 nyingine, nitafurahi sana."

Ureno inaongoza kundi A ikiwa na alama sita baada ya kuanza kampeni yako kwa ushindi dhidi ya Croatia ambayo imetulia katika nafasi ya pili baada ya kuifunga Poland 1-0 jana Jumapili.

Scotland imepoteza mechi mbili mfululizo ndani ya muda wa siku tatu huku kibarua cha kocha Steve Clark kikiwa hatarini kuota mbaya.