1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda kufanya uchaguzi mkuu siku ya Jumatatu

11 Julai 2024

Wananchi wa Rwanda watapiga kura siku ya Jumatatu, huku Rais Paul Kagame akitajarajiwa kushinda katika uchaguzi ambao unawashirikisha wagombea wale wale aliowashinda katika uchaguzi wa miaka saba iliyopita.

https://p.dw.com/p/4iBjE
Rwanda I Rais Paul Kagame akiwa katika kwenye kampeni za uchaguzi.
Rais Paul Kagame akiwa katika kwenye kampeni za uchaguzi anaotazamiwa kushinda kwa mara nyingine.Picha: Jean Bizimana/REUTERS

Kagame ambaye kimsingi ndiye amekuwa kiongozi wa Rwanda tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari mwaka 1994, anapambana na Frank Habineza, kiongozi wa chama cha Democratic Green, mgombea pekee wa upinzani aliyeidhinishwa kugombea, pamoja na Philippe Mpayimana anayesimama kama mgombea binafsi. 

Kagame ameshinda mara tatu kwa kupata zaidi ya asilimia 93 ya kura kwenye uchaguzi wa mwaka 2003, 2010, na 2017. Habineza alipata asilimia 0.48 katika uchaguzi wa mwaka 2017, huku Mpayimana akipata asilimia 0.73. 

Soma pia:Rwanda: Kagame kurejea madarakani kwa muhula wa nne?

Mapema mwaka huu mahakama za Rwanda zilitupilia mbali rufaa kutoka kwa wanasiasa maarufu wa upinzani Bernard Ntaganda na Victoire Ingabire, kuwafutia hukumu dhidi yao zilizotolewa awali, ambazo ziliwazuia kugombea katika uchaguzi. 

Jumla ya raia milioni 9.01 wa Rwanda wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi huo.