1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Safari za ndege za siri za CIA

8 Desemba 2005

Kashfa ya safari za ndege za siri za CIA na kunyakuliwa kwa raia wa kijerumani kunaendelea kugingwa vichwa vya habari katika magazeti ya Ujerumani:

https://p.dw.com/p/CHXd

Gazeti la TAZ linalochapishwa mjini Berlin laandika:

“Bibi Rice amezungumzia tu ni marufuku kwa maafisa wa usalama wa Marekani kutesa wafungwa hakujibu lakini swali iwapo raia wa nchi nyengine kwa niaba ya Marekani na ikibidi hata mbele ya maafisa wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, wakitesa wafungwa.Yeyote anaetupa macho ulimwenguni kwa matumaini ,sasa ana sababu ya kuhofia kuwa wafungwa wengi zaidi kuliko ilivyokua hadi sasa watanyakuliwa katika zile nchi ambazo Marekani ina uhuru wa kufanya itakavyo.”-ni maoni ya TAGES ZEITUNG kutoka Berlin.

Gazeti la Frankfurter Rundschau linatoa dhana kama hizo likiandika:

„Siku zilizopita Marekani ikipita mlango wa nyuma.Hatutesi wafungwa ,lakini tafsiri mpya ya kutesa jinsi ilivyobadilishwa ni vigumu kuitambua.Sasa Marekani inaelewa nini juu ya matamshi kama kuwatendea binadamu maovu na dhulma?

Je,tafsiri hii iwapige marufuku watumishi wa Marekani hata kukodi wahuni wanaotesa watu mradi wao tu hawafanyi hayo ?-lauliza FRANKFURTER RUNDSCHAU.

Ama gazeti la WESTFÄLISCHE RUNDSCHAU linaikodolea macho Ujerumani na kuona :

„Serikali ya Ujerumani haioneshi hamu kubwa katika kutoa habari.Kanzela anakwenda huku na kule katika duka la vikombe na sahani-kulia akiepuka kutonesha hisia za Marekani na kushoto kutowakera washirika wake katika serikali mpya ya muungano……..Katika kufanya hivyo, hataokoka.Kwani kila kukicha akiendelea na tabia hiyo ,kashfa hii inayohusu kutekwanyara kwa raia wa kijerumani na maajenti wa CIA,kunakigeuza kisa hiki kuwa kashfa ya serikali ya Ujerumani mjini Berlin.“ –ni uchambuzi wa WESTFÄLISCHE RUNDSCHAU.

Gazeti la DIE ZEIT kutoka Hamburg linatuarifu kuwa dai la upinzani bungeni kuunda Tume ya uchunguzi juu ya kisa cha misafara ya siri ya ndege za CIA katika viwwanja vya ndege vya Ujerumani,linaikuta serikali ya muungano ya Ujerumani katika wakati mbaya kabisa.Kwa kadiri rais wa sasa wa Marekani hajali kukiuka mamlaka ya dola nyengine ,haitawezekana kurejesha suluhu ya kweli kati ya Washington na Berlin –laandika DIE ZEIT.

Likiendelea mada hii kwa upande mwengine,gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG kutoka Munich linatuuzindua kwamba mawaziri 4 wa serikali iliotangulia hii walipashwa habari juu ya kunyakuliwa kwa raia wa kijerumani El Masri na shirika la ujasusi la Marekani CIA:SDZ laandika:

„Alao tangu jana kunyakuliwa kwa El masri si mkasa unaoihusu serikali iliopita.Sasa pia ni kisa cha Kanzela wa serikali ya sasa.Kwa kusisitiza kwake kuwa Marekani imekubali kunyakuliwa kwa El Masri lilikua kosa,Kanuzela anajikuta kati ya kuonesha ujabari na wakati huo huo woga.Yadhihjirika, taarifa zake amezipata kutoka kwa waziri wa nje wa Marekani bibi Rice ambae haungami kuzungumza nae chochote cha aina hiyo.“

Likitumalizia mkasa huu,gazeti la REUTLINGER-ANZEIGER likimtaja waziri wa ndani Otto Schilly na jinsi alivyohusika na kunyakuliwa kwa raia wa Ujerumani El Masri,laandika:

„Yafaa kusikiliza nini asema waziri wa zamani wa mambo ya ndani Otto Schilly juu ya mkasa wa El Masri:anadai alijulishwa kisa chake wakati ambao hangeweza kufanya lolote.Uzuri basi kwake.“