Juhudi za wabunge wa Kenya kumuondoa madarakani naibu wa rais Rigathi Gachagua zilihamia haraka katika baraza la seneti (09.10.2024) baada ya bunge la kitaifa kupiga kura kuunga mkono hoja ya kumuondoa. Je sakata hili linawezaje kubadili mkondo wa siasa za taifa hilo la Afrika Mashariki? Jiunge na Josephat Charo katika Maoni mbele ya Meza ya Duara.