1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia yalaani mashambulio ya anga ya Israel, Rafah

29 Mei 2024

Saudi Arabia imelaani mashambulio ya anga yaliyofanywa na Israel mjini Rafah. Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo imesema serikali inalaani mauaji ya halaiki yanayofanywa na vikosi vya Israel kwa Wapalestina

https://p.dw.com/p/4gPhs
Saudi Bin Salman
Kiongozi wa Saudia, mwanamfalme Mohammed Bin SalmanPicha: Saudi Press Agency/dpa/picture alliance

Riyadh imesema Israel inabeba dhamana kwa kinachotokea Rafah na kwenye maeneo yote inayoyakalia ya ardhi ya Wapalestina.

Kadhalika imesema hatua ya Israel ya kuendelea kukiuka maazimio ya kimataifa na kuhusu hali ya kibinadamu,inaongeza ukubwa wa janga linalowakabili Wapalestina.

Saudi Arabia yalaani mashambulizi ya Israel huko Rafah

Wakati huohuo jeshi la Israel imesema wanajeshi wake watatu wameuliwa katika mapigano Kusini mwa Gaza leo Jumatano,wakati likiendelea na operesheni yake Rafah.

Wanajeshi wengine watatu walijeruhiwa vibaya katika tukio hilo hilo.Hata hivyo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa na Israel kuhusu tukio hilo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW