SiasaSaudi Arabia
Saudi Arabia yaukaribisha ujumbe wa Iran na Syria
13 Aprili 2023Matangazo
Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imesema waziri wa mambo ya nje wa Syria Faisal Mekdad amekutana na mwenzake wa Saudi Arabia na kujadili kwa kina hatua za kuchukua ili kufikia suluhu kamili ya kisiasa katika mgogoro wa Syria, lengo likiwa ni kupata muafaka wa kitaifa na kulirejesha taifa hilo katika ulimwengu wa Kiarabu.
Soma pia: Ujumbe wa Iran wazuru Saudia kusawazisha mahusiano
Wakati hayo yakijiri Rais wa Iran Ebrahim Raisi anatarajiwa nchini Saudi Arabia hivi karibuni, huku taifa hilo likiendelea na majadiliano na waasi wa Kihouth katika kukomesha mapigano huko Yemen, hatua iliyozidi kuongeza matumaini ya kuleta utulivu katika mataifa ya Ghuba.