1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz aahidi kuwalinda Wayahudi dhidi ya vitendo vya chuki

9 Novemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameapa leo kuwa atawalinda Wayahudi dhidi ya chuki inayoongozeka tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas huko Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4YcqU
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: John Macdougall via REUTERS

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametoa ahadi hiyo wakati akihutubia hafla ya kumbukumbu ya miaka 85 tangu kuzuka kwa wimbi la chuki na ubaguzi dhidi ya Wayahudi vilivyopelekea kutokea mauaji ya halaiki ya wayahudi, Holocaust, chini ya utawala wa Manazi wa Ujerumani.

Maadhimisho hayo yamefanyika kwenye sinagogi moja mjini Berlin ambalo lililengwa na washambuliaji mnamo mwezi uliopita baada ya Israel kuanza operesheni yake ya kijeshi kwenye Ukanda wa Gaza kujibu shambulizi la kundi la Hamas la Oktoba 7.

Tangu wakati huo matukio yasiyopungua 2,000 ya chuki dhidi ya Wayahudi yameripotiwa nchini Ujerumani na serikali imelazimika kuongeza ulinzi kwenye taasisi za kiyahudi.

Scholz ameyataja matukio hayo kuwa "fedheha" na amesema serikali mjini Berlin itafanya kila inachoweza kuyadhibiti.