1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz aitembelea Solingen baada ya shambulizi la kisu

26 Agosti 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amewasili katika mji wa Solingen magharibi mwa nchi hiyo mapema hii leo, ikiwa ni siku tatu baada ya shambulizi baya la kisu kwenye eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4jvDn
Ujerumani Solingen | Olaf Scholz
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani akiwasili kwenye ofisi za mji wa Solingen kutoa pole na kupokea maelezo juu ya shambulizi la kisu lililowaua watu watatu. Picha: Henning Kaiser/REUTERS

Scholz alikaribishwa na meya wa Solingen, Tim Kurzbach, na kuungana na Hendrick Wüst, Waziri Mkuu wa Jimbo la Norh Rhine Westphalia ambako mji huo unapatikana, Naibu Waziri Mkuu Mona Neubaur na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Jimbo Herbert Reul.

Baada ya mkutano wa maafisa hao katika ofisi ya jiji, kutafanyika shughuli ya kuwakumbuka wahanga katikati ya jiji, kulikotokea shambulizi.

Scholz pia atazungumza na watumishi wa huduma za dharura.

Mtu mmoja, raia wa Syria, ametiwa nguvuni kwa tuhuma za kuwashambulia watu waliokuwa kwenye sherehe siku ya Ijumaa na kuwaua watatu na kuwajeruhi wanane.