1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz asema hatokuwa naibu kansela iwapo Merz atashinda

12 Desemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, amesema hatokuwa makamu wa kansela chini ya serikali ya mpinzani wake wa kihafidhina Friedrich Merz, kufuatia uchaguzi wa mapema uliopangwa kufanyika mwezi Februari.

https://p.dw.com/p/4o4iE
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.Picha: Carsten Koall/dpa/picture alliance

Scholz ambaye alikuwa makamu wa kansela chini ya serikali ya Angela Merkel, na anayegombea tena katika nafasi ya ukansela, amekiambia leo kituo cha redio cha Ujerumani cha Deutschlandfunk kwamba hatokuwa makamu wa Merz.

Uchaguzi wa Ujerumani unatarajiwa kufanyika Februari 23, 2025, baada ya serikali ya muungano wa vyama vitatu chini ya Kansela Scholz kuvunjika mwanzoni mwa mwezi Novemba.

Jana, Scholz aliwasilisha rasmi mbele ya bunge ombi la kuitisha kura ya imani, itakayofungua njia ya kufanyika uchaguzi wa mapema wa bunge.

Kura hiyo inatarajiwa kupigwa Jumatatu ijayo.