1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schröder na Chirac wazungumzia ugaidi na katiba ya UU.

16 Machi 2004
https://p.dw.com/p/CFec

PARIS: Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani na Rais Jacques Chirac wa Ufaransa wanahimiza mkakati wa pamoja wa kupigana na ugaidi katika nchi za UU. Kufuatana na yale mashambulio ya Uspania, magaidi sasa wamekwisha jizatiti barani Ulaya, alisema Kansela Schröder, baada ya mazungumzo yake pamoja na Rais Chirac mjini Paris. Upande wake Rais Chirac alitoa mwito wa kumalizwa migogoro ya kimataifa ambayo alisema ni chanzo cha mashambulio ya kigaidi, hasa hasa mgogoro wa Mashariki ya Kati. Kansela Schröder alisema ana matumaini kuwa katiba ya UU itaweza kusainiwa wakati bado Ireland imeshika wadhifa wa Rais wa UU hadi hapo mwishoni mwa Juni. Naye Waziri Mkuu mteule wa Uspania José Luis Zapatero ametamka katika risala ya simu niya yake ya kutaka ushirikiano wa karibu na Ujerumani na Ufaransa.