1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SCHROEDER ZIARANI AFRIKA:

19 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFhg
ADDIS ABABA: Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amekutana na waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi mjini Addis Ababa akiwa mwanzoni mwa ziara yake ya siku sita barani Afrika.Wakati wa mkutano huo Schroeder na Zenawi walizungumza juu ya ushirikiano wa kiuchumi na sera ya usalama.Schroeder ameahidi kuisaidia serikali ya Ethiopia katika utaratibu wa kidemokrasia.Hasa msaada huo utahusika na mafunzo ya ufundi na kuanzishwa kwa uhuru wa vyombo vya habari.Ujerumani na madola mengine yanaitaka Ethiopia ichukue hatua zaidi kuumaliza mzozo wake na nchi jirani Eritrea.Schroeder anatazamiwa pia kutoa hotuba muhimu katika makao makuu ya Umoja wa Afrika-AU kuhusu siasa ya Ujerumani barani Afrika.Ujerumani hutoa Euro milioni kadhaa kuusaidia Umoja wa Afrika katika juhudi zake za amani na usalama.