1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SCHROEDER ZIARANI BARA AFRIKA:

18 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFi3
BERLIN: Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani hii leo ameanza ziara yake ya wiki moja barani Afrika.Ziara hiyo itampeleka Ethiopia Kenya,Afrika ya Kusini na Ghana.Kwa mujibu wa duru za ofisi ya Kansela,masuala yatakayochukua nafasi muhimu yanahusika na misaada ya maendeleo na sera za usalama.Wakati wa ziara hiyo Schroeder ataahidi msaada mkubwa wa Ujerumani ikiwa nchi hizo zitajitahidi kuleta udemokrasi zaidi na zitaimarisha uchumi wao.Kansela Schroeder amefuatana na tume ya wataalamu 23 wa kiuchumi,hasa wakiwa ni wakuu wa makampuni ya wastani na pia wakubwa wa Daimler-Chrysler na Lufthansa.