Schröder ameridhika na ziara yake ya Marekani
28 Februari 2004Matangazo
WASHINGTON: Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani amesema ameridhika na ziara yake nchini Marekani. Anafikiri ilikuwa ziara muhimu iliyofanyika wakati muwafaka, alisema Bwana Schröder. Pia alisema amefurahishwa na yale mazungumzo yake pamoja na Rais George W. Bush. Muhimu sasa ni kutazama mbele, alisisitiza Kansela. Kuhusu mada ya mabishano ya zamani juu ya vita vya Iraq, Kansela alisema, Rais Bush hakuwa na madai yoyote kwa Ujerumani, bali kinyume cha mambo ametoa heko kwa mchango wa Ujerumani nchini Afghanistan. Uamuzi wa Ujerumani kwamba haina niya ya kupeleka wanajeshi wake Iraq unajulikana na kuheshimiwa na Marekani. Kwake yeye, ziara hiyo imemaliza mabishano kati ya Marerakni na Ujerumani kuhusu vita vya Iraq, alisisitiza Kansela Schröder. Ilikuwa ziara ya kwanza ya Kansela wa Ujerumani kufanyika Washington tangu miaka miwili. Iraq yaomba msaada wa dharura wa Dollar biliyoni nne.