1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schröder na Chirac wazungumzia ugaidi na katiba ya UU.

16 Machi 2004
https://p.dw.com/p/CFei

PARIS: Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani na Rais Jacques Chirac wa Ufaransa wanashauriana hii leo juu ya mkakati wa kupigana na ugaidi na juu ya katiba ya Umoja wa Ulaya (UU). Kufuatana na yale mashambulio ya kigaidi nchini Uspania, viongozi hao wawili wanahimiza kuwa nchi za UU ziwiyanishwe harakati zao za kupigana na ugaidi. Katika mjadala kuhusu swali la kutiwa makali hatua za kupigana na ugaidi, Kansela Schröder amesisitiza tena kuwa anapinga madai ya upinzani kuwa wanajeshi wa Kijerumani watumiwe kwa wingi katika hifadhi ya usalama wa ndani. Mazungumzo hayo mjini Paris yanasisitiza ziendelezwe juhudi za kufikiwa uwiyano juu ya katiba ya UU. Serikali mpya ya Kisoshalisti mjini Madrid inataka kubatilisha ule msimamo wa Uspania wa kuiwekea vizingiti katiba ya UU. Mkutano huo unahudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean-Pierre Raffarin na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Joschka Fischer.