1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSerbia

Serbia na Kosovo zakubali mpango wa kurejeshea uhusiano

28 Februari 2023

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic na Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti wamekubali pendekezo la Umoja wa Ulaya kurejesha mahusiano yao ya kidiplomasia yaliyokumbwa na mivutano ya muda mrefu.

https://p.dw.com/p/4O4Mu
Belgien l EU-Gespräche in Brüssel mit Kurti, Vucic und Borrell
Picha: Virginia Mayo/AP/picture-alliance

Akizungumza baada ya mazungumzo ya upatanishi mjini Brussels jana, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema mazungumzo zaidi sasa yanahitajika ili kuutekeleza mpango huo ambao huenda ukakamilishwa ifikapo mwisho wa mwezi Machi. Borrell amesema pande zote zimeapa kutochukua hatua za upande mmoja zinazoweza kusababisha mivutano na kuyahujumu makubaliano hayo.

Miongoni mwa mengi yaliyokubaliwa, muafaka huo unawapa fursa watu kusafiri kwa uhuru kati ya Kosovo na Serbia kwa kutumia paspoti zao, vitambulisho na vibao vya nambari za usajili wa magari. Borrell amesema makubaliano hayo yanaweza kufungua fursa mpya za kiuchumi na kuvutia uwekezaji nchini Kosovo na Serbia.