1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serika ya Kenya yakataa kufanya mazungumzo na upinzani

Thelma Mwadzaya30 Machi 2023

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amewaongoza mamia ya wafuasi wake katika duru nyingine ya maandamano makubwa ya umma kuishinikiza serikali kushughulikia kadhia ya kupanda kwa gharama za maisha.

https://p.dw.com/p/4PWJK
Kenia | Ausschreitungen und Proteste in Nairobi und Kisumi
Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Msafara wa kiongozi wa upinzani wa Azimio la Umoja One Kenya unaoongozwa na Raila Odinga ulitua kwanza mtaani Muthurwa baada ya kupitia barabara kuu ya Mombasa. Aliuhutubia umma, kiongozi wa upinzani Raila Odinga alisisitiza kuwa kamwe hawatolegeza msimamizi hadi serikali iwasikilize.

Hii ni wiki ya pili ya maandamano ya kitaifa . Hii leo Azimio wameitimiza ahadi yao ya kukusanyika mara mbili kila wiki kuishinikiza serikali kuishusha gharama ya maisha.

Upinzani wa Kenya waishutumu serikali kwa kuchochea matabaka

Juhudi za wanasiasa hao wa upinzani na wafuasi wao kuingia kwenye eneo la katikati ya jiji la Nairobi halikufua dafu kwani maafisa wa usalama walikuwa wanadhibiti sehemu zote za kuelekea humo.

Wakati huohuo, Rais William Ruto amerejea nyumbani mapema hii leo baada ya ziara ya siku nne ya Ujerumani na Ubelgiji.Kwenye kongamano la biashara kati ya Marekani na Kenya, AMCHAM,Rais Ruto alitangaza mipango mipya ya kuimarisha sekta hiyo.

Ruto atetea rikodi yake licha ya maandamano ya upinzani

Kwa upande wake, idara ya polisi imezipuuzilia mbali ripoti za mitandao ya jamii zinazowanyoshea kidole cha lawama kwa kusababisha vurugu wakati wa maandamano hayo ya amani.Kwenye taarifa yake,idara ya polisi ya Kenya, NPS, ilibainisha kuwa madai hayo sio ya kweli na ni ya kupotosha huku lengo lake likiwa ni kuiharibia sifa. Idara hiyo ya polisi inasisitiza kuwa wajibu wake ni kuwalinda wakenya wote.

Licha ya Maandamano Kenya yasifika kwa ustawi wa demokrasia

Berlin Präsident William Ruto Kenia im DW-Interview
Rais wa Kenya William Ruto Picha: DW

Yote hayo yakiendelea,Kenya imepongezwa na mataifa 8 ya kigeni kwa kuwa nanga ya ustawi, usalama na demokrasia barani Afrika kufuatia uchaguzi mkuu wa amani uliokuwa na ushindani mkubwa.

Hata hivyo mabalozi wa Canada, Marekani, Australia, Uholanzi, Denmark, Sweden na Uingereza wameelezea wasiwasi wao mintarafu vurugu na uharibifu wa mali ulioshuhudiwa kwenye baadhi ya maeneo wakati wa maandamano ya kitaifa yanayoendelea.

Kenya, Ujerumani kuondowa vikwazo vya ushuru

Muda mfupi uliopita,naibu wa rais Rigathi Gachagua, aliyeongoza hafla ya mabaharia 500 waliofuzu Mombasa amebainisha kuwa mazungumzo watakayoweza kufanya na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ni kuhusu jinsi atakayolihama jukwaa la siasa za Kenya.Kwa mtazamo wake Raila Odinga hajawatendea haki wakenya.

Mwandishi: Thelma Mwadzaya