Serikali mpya ya Tunisia yakutana
21 Januari 2011Matangazo
Mkutano huo umefanyika huku maandamano mapya ya kutaka kuondolewa viongozi wa serikali iliyopita ya rais aliyeondolewa madarakani, Zine El Abidine Ben Ali, yakiendelea.
Mawaziri hao wamekubaliana kutoa msamaha kwa wafungwa wote wa kisiasa na kuvihalalisha vyama vya siasa na makundi yaliyokuwa yamepigwa marufuku.
Wakati huo huo, polisi katika mji mkuu wa Tunis, wamefyatua risasi za onyo kuwatawanya mamia ya waandamanaji karibu na makao makuu ya kilichokuwa chama tawala.
Mmoja kati ya wapinzani wakuu wanaoongoza nchini humo, Taoufik Ben Brik, ametangaza kugombea katika uchaguzi wa rais ambao serikali ya mpito imesema utakuwa huru na wa haki.