1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ulimwenguni zawasiliana na watawala wapya wa Syria

16 Desemba 2024

Serikali mbali mbali za ulimwengu zimeongeza juhudi za kuanzisha mawasiliano na watawala wapya wa Syria.

https://p.dw.com/p/4oC84
Syrien |  Damaskus Feierlichkeiten zum Sturz von al-Assad
Picha: SAMEER AL-DOUMY/AFP/Getty Images

Hatua hiyo inachukuliwa zaidi ya wiki moja baada ya waasi wa msimamo mkali wa kiislamu kumuangusha madarakani rais Bashar al-Assad na kuondowa utawala wake wa kikatili na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Jana mjumbe wa Umoja wa Mataifa Geir Pederson alikuweko Damascus ambako alitowa mwito wa kuundwa serikali itakayowajumuisha watu wote na itakayojikita katika kuijenga mpya nchi hiyo na kuleta haki.

Alikutana na kiongozi wa HTS Ahmed al Sharaa na kumtolea mwito wa kutenda haki na kuwawajibisha waliofanya uhalifu.

Qatar ambayo kesho inafungua rasmi ubalozi wake Damascus pia ni miongoni mwa nchi ambazo zilipeleka ujumbe wake Syria jana kukutana na serikali ya mpito.

Hatua ya Qatar inakuja baada ya Jumamosi Uturuki nayo kufungua ubalozi wake Damascus.

Marekani na Uingereza pia zimethibitisha kuwa na mawasiliano na uongozi wa HTS hlicha ya kuliweka kundi hilo katika orodha ya makundi ya kigaidi,huku Umoja wa Ulaya ukitangaza kumtuma mjumbe wake Syria hii leo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW