Ethiopia yapiga marufuku mashirika 3 ya haki za binadamu
3 Desemba 2024Shirika hilo limeishurumu nchi hiyo kuzima fursa ya mwisho ya kuwepo uangalizi huru katika wakati ambapo kuna mgogoro unaozidi kuwa mbaya.
Ethiopia ilichukuwa hatua ya kuzuia kazi za mashirika ya CARD, AHRE na LHR tangu Novemba 14 ikisema mashirika hayo yana upendeleo wa kisiasa na yanavuruga maslahi ya nchi hiyo.
HRW: Umoja wa Mataifa uchunguze mauaji ya jeshi la Ethiopia
Naibu mkurugenzi wa shirika la Human Rights Watch Laetitia Bader, amesema hatua hiyo ya serikali ya Addis Ababa, inaonesha kwamba nchi hiyo bado inabakia kuwa miongoni mwa maeneo hatari yasiyovumilia ukosoaji wa vitendo vya serikali na kujali haki za binadamu.
Mashirika yaliyopigwa marufuku, yanayodai kutoegemea upande wowote kisiasa, yalilengwa muda mfupi baada ya kusaini barua ya wazi iliyokosoa mapendekezo ya kufanya mageuzi katika sheria ya vyombo vya habari nchini humo.