Pamoja na mkataba wa uwekezaji wa bandari ya Dar es Salaam kati ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai kupingwa na makundi mbalimbali, serikali ya taifa hilo inasema inaandaa nyaraka kwa ajili ya utekelezaji wa makubaliano kamili ya kisekta ya mkataba huo, ingawa msemaji mkuu, Gerson Msigwa, ameiambia DW kwamba serikali inaendelea kuyapokea maoni ya wakosoaji wake na kuyafanyia kazi.