1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Ufaransa yakabiliwa na kitisho cha kuangushwa

4 Desemba 2024

Wabunge wa Ufaransa watapiga hii leo kura ya kutokuwa na imani na serikali, ambayo huenda ikaiondosha serikali ya Waziri Mkuu Michel Barnier na kulitumbukiza taifa hilo kwenye mzozo mkubwa wa kisiasa.

https://p.dw.com/p/4nkKC
Michel Barnier
Waziri Mkuu Michel Barnier Picha: Alexandre Marchi/MAXPPP/dpa/picture alliance

Hoja hiyo iliyowasilishwa bungeni na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally cha Marine Le Pen hata hivyo inatarajiwa kukataliwa. Lakini Le Pen amesema washirika wake wataipa kura za kutosha kupitishwa katika mchakato huo wa leo jioni unaotarajiwa kuiangusha serikali kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 60. Barnier mwenyewe amesema jana kwenye mahojiano yaliyorushwa kwenye televisheni kwamba anaamini serikali yake itakivuka kihunzi hicho.