Serikali ya Ujerumani yaisifu maendeleo Ujerumani Mashariki
22 Novemba 2013Moja ya malengo ya sera zinasozifiwa Ujerumani ni usawa wa hali ya maisha ya watu katika maeneo yote ya nchi, hali ambayo ilikuwa changamoto kubwa kwa Ujerumani Magharibi, kutokana na kuwepo kwa tofauti kubwa kati ya Kaskazini na kusini.
Pallipo na mwanga, pana kivuli,ndivyo inavyoanza ripoti hiyo, Ripoti mpya imetolewa na serikali ya Ujerumani ikiiangalia Ujerumani Mashariki kwa mtazamo chanya, ikiwa ni miaka 23 baada ya kuungana, huku kukiwa bado kuna tofauti kati ya Magharibi na Mashariki.
Serikali ya Ujerumani ilijidhatiti kuwa itakuwa ikitoa ripoti za mara kwa mara kuhusu maendeleo ya Muungano, ambapo kwa mara ya kwanza ripoti ya mwaka huu iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani imeonyesha kuwa watu wa Ujerumani Mashariki wanajuhudi zaidi kuliko ilivyo kwa wale wa Magharibi.
Mabadiliko makubwa tangu kuunga 1990
Hata hivyo tangu kuungana kwa pande hizo mbili mwaka 1990, kulitokea mabadiliko makubwa, ambapo majimbo mapya makubwa matano ambayo awali yaliiunganisha Ujerumani Mashariki yalikuwa masikini, lakini baada ya miaka 40 ya utawala wa kikomunisti, kansela wa wakati huo, Helmut Kohl aliahidi kuwepo kwa matumaini ya muungano, ingawa mwaka uliofuatia Mashariki ilikabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira na kuporomoka kwa viwanda.
Na tangu kuungana, Ujerumani Mashariki imepoteza makaazi milioni 2, au asilimia 13.5 ya wakaazi wake, ikiwa wengi walihamia upande wa Magharibi kwa ajili ya kutafuta ajira, jambo ambalo waziri wa Dola wa Ujerumani, Christoph Berner amesema hali hiyo sasa imeimarika.
Anasisitiza waziri huyo kuwa, kwa sasa vijana kati ya umri wa miaka 30 hadi 40 waliohama wakati huo, sasa wameanza kurejea kwao , kwa kuwa ni rahisi sasa kupata kazi.
Waziri huyo anasema wengi wapo tayari kupata mshahara wa kiwango cha chini, ili mradi kuungana na familia zao na marafiki, au kutokana na kuthamini eneo walikotoka.
Wastani wa kuishi waongezeka
Kwa mara ya kwanza pia ripoti hiyo imeeleza kwamba kwa upande wa elimu wanafunzi kutoka Ujerumani Mashariki wanafanya vizuri, wakati wastani wa kuishi umeongezeka zaidi ya ule wa Ujerumani Magharibi, kutokana na kuboreshwa kwa huduma za matibabu na kupungua kwa uchafuzi.
Jambo jingine linalosifisiwa ni uwiano wa wahamiaji, kuongezeka kwa vyuo vya elimu ya juu na vyuo vikuu vyenye vifaa vya kutosha na kuvutia wanafunzi kutoka Ujerumani Magharibi, lakini pia kuwepo kwa taasisi za utafiti.
Uchumi pia umekuwa, ambapo Waziri wa mambo ya ndani w Ujerumani, Hans-Peter Fredirich anasema uimara katika uchumi bado ni asili mia 71na hivyo kushindana katika ngazi ya kimataifa.
Kuwepo kwa viwanda vya uzalishaji, na miundo mbinu ya kisasa, njia bora za usafiri, ni maendeleo ambayo yanatajwa, kitu ambacho Ujerumani Magharibi, inapaswa kujifunza.
Ingawa pande zote za Ujerumani zinajitahidi, hata hivyo tofauti bado zipo huku watu wa upande wa Mashariki wakifanya vizuri zaidi, lakini bado kuna tofauti katika usawa wa kimifumo.
Mwandishi: Flora Nzema
Mhariri: Sumu Yusuph Mwasimba