1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la Magdeburg lachukua mkondo mpya wa kisiasa

23 Desemba 2024

Shambulio kwenye soko la Krismasi huko Magdeburg, ambapo watu watano waliuawa limechukua mkondo mpya wa kisiasa nchini Ujerumani ambapo chama cha AFD na wapinzani wake wanapanga kufanya maandamano.

https://p.dw.com/p/4oVZy
Magdeburg
Maua yaliyowekwa na waombolezaji huko MagdeburgPicha: Klaus-Dietmar Gabbert/dpa/picture alliance

Shambulio kwenye soko la Krismasi huko Magdeburg, ambapo watu watano waliuawa siku ya Ijumaa limechukua mkondo mpya wa kisiasa nchini Ujerumani ambapo chama cha mrengo mkali wa kulia cha AFD na wapinzani wake wanapanga kufanya maandamano leo Jumatatu.

AFD inapanga kufanya maandamano hayo katika mji wa Domplatz uliopo mashariki mwa Ujerumani. Mgombea wa ukansela wa chama hicho katika uchaguzi wa mwezi Februari Alice Weidel na wanasiasa kadhaa wa chama hicho katika ngazi ya jimbo watahudhuria huku suala la uhamiaji linatarajiwa kuangaziwa katika maandamano hayo.

Soma zaidi. Serikali kuanzisha uchunguzi baada ya shambulio la Magdeburg

Kwa upande mwingine, maandamano ya kuonesha mshikamano yanayobeba kaulimbiu ya "Epusha chuki" yanapanga kufanyika karibu na soko la Krismasi ambako mwanaume mmoja mwenye asili ya Saudi Arabia alilivurumisha gari na kuuparamia umati wa watu kwa makusudi siku ya Ijumaa. 

Mkasa huo uliowajeruhi zaidi ya watu wengine 200 umezusha simanzi kubwa nchini Ujerumani na kuzidisha makali kwenye mjadala kuhusu sera ya uhamiaji.