MigogoroUlaya
Urusi: Ukraine imeshambulia Zaporizhzhia na kuuwa watu 16
14 Aprili 2024Matangazo
Hayo yameelezwa leo na Afisa aliyeteuliwa na Urusi katika mkoa huo wa kusini mwa Ukraine Yevgeny Balitsky na kusisitiza kwamba watu 20 wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi hayo ya usiku wa Ijumaa, na 12 wana hali mbaya.
Shirika la habari la Reuters hata hivyo halikuweza kuthibitisha taarifa hizi, na Ukraine haijasema chochote juu ya madai haya. Moscow na Kyiv wamekuwa wakituhumiana kufanya mashambulizi eneo hilo.
Zaporizhzhia ni moja ya mikoa minne ya Ukraine iliyokuwa ikikaliwa kwa kiasi fulani na wanajeshi wa Urusi na ambayo Moscow iliyanyakua baada ya kuivamia kikamilifu Ukraine Februari mwaka 2022.