1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Shambulio la Urusi lauwa watu 6 Zaporizhzhya

5 Novemba 2024

Watu sita wameuawa kutokana na mashambulizi ya makombora ya Urusi katika mji wa kusini mashariki mwa Ukraine wa Zaporizhzhya. Haya ni kwa mujibu wa maafisa mjini humo.

https://p.dw.com/p/4mejM
Athari za shambulio la Urusi Ukraine
Athari za shambulio la Urusi UkrainePicha: Serhii Chuzavkov/Ukrinform/IMAGO

Ivan Federov ambaye ni mkuu wa jeshi eneo hilo amesema idadi ya waliojeruhiwa kutokana na shambulizi hilo imeongezeka na kufikia watu 16, ingawa afisi ya mwendesha mashtaka mkuu mjini Kyiv imesema kwamba watu 20 ndio waliojeruhiwa.

Hayo yakiarifiwa mkuu wa kukabiliana na usambazaji wa habari za uongo katika baraza la usalama la Ukraine, Andrii Kovalenko, amesema kuwa vikosi vya Korea Kaskazini vilivyotumwa kuisaidia Urusi katika vita tayari vimeshambuliwa na jeshi la Ukraine.

Soma pia:Zelensky adai wanajeshi 11,000 wa Korea Kaskazini wako Kursk

Kovalenko ameyaandika hayo katika mtandao wa kijamii wa Telegram ila hakutoa taarifa zaidi. Taarifa za kiintelijensia za Marekani, Korea Kusini na Ukraine zinasema kuwa Pyongyang imetuma kikosi cha wanajeshi 12,000 katika vita hivyo katika mkataba na Urusi.