1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shikika la KidsRight: Haki za watoto zazidi kukiukwa duniani

17 Julai 2024

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za watoto la KidsRights limesema haki za watoto zinazidi kumomonyoka kutokana kuongezeka ka migogoro ya silaha duniani kote, ikiwa ni pamoja na vita vya Gaza, Sudan na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4iPMg

Katika ripoti yake ya kila mwaka shirika hilo, ambalo huandaa Tuzo ya Kimataifa ya Amani ya Watoto limesema kumekuwa na ongezeko la asilimia 21 ya ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto katika migogoro ya silaha duniani kote" tangu mwaka jana na kutoa wito wa kuboresha ulinzi wao.

Ukiukaji huo unajumuisha mauaji na kuwasababishia ulemavu watoto, pamoja na kuajiri na kutumia askari watoto, utekaji nyara, na kunyimwa msaada wa kibinadamu.

UNICEF yasema watoto karibu watoto 300,000 wahama makwao nchini Haiti

Marc Dullaert, mwanzilishi na mwenyekiti wa KidsRights, amesema ripoti hiyo inaangazia athari mbaya za mzozo kwa watoto na haki zao, hatua ambayo inadhoofisha miongo kadhaa ya maendeleo.

Dullaert ametoa wito kwa serikali kukabiliana na ukweli kwamba Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa yanayohusiana na haki za watoto, ikiwa ni pamoja na kumaliza umaskini na njaa, na upatikanaji wa elimu, hayana uwezekano wa kufikiwa.

Ripoti hiyo imeiorodhesha Luxemburg kuwa nchi inayoongoza kwa kulinda haki za watoto, huku Afghanistan ikishika nafasi ya mwisho.