1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMarekani

Delta Air Lines yasitisha safari za ndege kwenda Israel

20 Septemba 2024

Shirika la ndege la Delta Air Lines nchini Marekani limetangaza kusitisha safari za moja kati ya New York na Tel Aviv hadi mwisho wa mwaka kutokana na kuongezeka kwa mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/4ksTr
Delta Airline Flug I Flugzeug
Picha: Nicolas Economou/NurPhoto/picture alliance

Shirika hilo la ndege kupitia taarifa limesema abiria walioathirika wanaweza kukata upya tiketi za ndege kuanzia Machi 1, mwaka 2025.

Delta Air Lines inaungana na mashirika mengine ya ndege ambayo pia yamefuta au kusitisha safari za ndege katika siku za hivi karibuni kwenda katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwemo miji ya Beirut na Tehran, kufuatia mapigano kati ya Israel na kundi la Hezbollah.

Soma pia: Hezbollah yavurumisha makombora dhidi ya Israel

Uamuzi huo wa Delta Air Lines unamaanisha kuwa shirika hilo limesitisha safari zote za moja kwa moja kati ya Marekani na Israel hadi mwisho wa mwaka huu.

Mashirika mengine ya ndege ikiwa ni pamoja na Air France, Lufthansa na Swiss pia yamesitisha kwa muda safari zao za ndege kwenda Israel.