IMF yasema uchumi wa dunia unaendelea vizuri
26 Julai 2023Shirika la fedha la kimataifa IMF limesema uchumi wa dunia unaendelea vizuri lakini ustawi ni dhaifu na bado pana wasiwasi. Kuhusu uchumi wa Ujerumani, shirika hilo la fedha la kimataifa IMF limesema limeteremsha matarajio kwa sababu uchumi wa Ujerumani utanywea kwa asilimia 0.2.
Uchumi wa dunia unatarajiwa kustawi kwa asilimia 0.2 mwaka huu
Kulingana na utabiri uliochapishwa mjini Washington, uchumi wa dunia unatarajiwa kustawi kwa asilimia 0.2 hadi asilimia 0.3 mnamo mwaka huu. Hata hivyo mtaalamu mkuu wa uchumi wa shirika la IMF ametahadharisha kwamba bado yapo matatizo na kwamba ni mapema mno kusherehekea. Amesema mfumuko wa bei unaendelea kusababisha wasi wasi na kwa ajili hiyo shirika la fedha la kimataifa linapendekeza kuendelea na mkakati wa kupandisha viwango vya riba.