Shirika la Oxfam laelezea mashaka ya hali ya kiutu Gaza
23 Desemba 2024Matangazo
Oxfam imesema hali hiyo inaibua wasiwasi juu ya hali mbaya ya kibinadamu katika eneo lililozingirwa la Palestina. Israel imeipinga ripoti hiyo, ikisema imetolewa makusudi na isivyo sahihi kwa nia ya kupuuza juhudi za serikali ya Israel za kufikisha misaada ya kibinadamu Gaza. Wizara ya afya katika Ukanda waGaza inayoendeshwa na Hamas imesema siku ya watu 58 wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita, na kufanya idadi ya vifo katika vita hivyo kufikia watu 45,317. Wizara hiyo pia imesema kwamba watu zaidi ya laki moja na saba wamejeruhiwa katika vita vya zaidi ya miezi 14 kati ya Israel na kundi la Hamas, baada ya mashambulio yake ya Oktoba 7, mwaka 2023 katika ardhi ya Israel.