UNRWA yasitisha shughuli zake kufuatia wasiwasi wa usalama
1 Desemba 2024Mkuu wa shirika hilo amesema barabara ya eneo hilo sio salama kwa kipindi cha miezi kadhaa sasa. Phillipe Lazzarini amesema kupitia ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa X kwamba msafara wa malori ya msaada ulivamiwa na kuporwa na magenge ya watu wenye silaha jana wakati wakijaribu kupeleka msaada kupitia njia hiyo. Mkuu huyo wa UNRWAameonya kwamba njaa inaongezeka katika ukanda wa Gaza. Ameitaka Israel kuhakikisha msaada unaingia katika Ukanda wa Gaza kwa kujizuia kushambulia wafanyakazi wa kutowa msaada wa kibinadamu. Jana shambulio la Israel liliwauwa wafanyakazi watatu wa shirika la msaada la Marekani la World Central Kitchen, akiwemo mmoja ambaye jeshi la Israel limesema alihusika kwenye uvamizi wa Oktoba 7, 2023 uliofanywa na Hamas.