1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

UNESCO yaonya kuhusu uporaji katika makumbusho Sudan

Angela Mdungu
12 Septemba 2024

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, limetahadharisha juu ya ripoti za uwepo wa makundi ya watu wenye silaha wanaopora na kuharibu nyumba za makumbusho na taasisi za utamaduni nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4kYk1
Moja ya mitaa ilioshambuliwa vibaya zaidi Sudan
Moja ya mitaa ilioshambuliwa vibaya zaidi SudanPicha: Mudathir Hameed/dpa/picture alliance

Uporaji uliotajwa katika ripoti hiyo umefanyika katika Makumbusho ya taifa ya Sudan, Makumbusho ya Khalifa huko Omdurman na ya Nyala Kusini mwa jimbo la Darfur.

Soma pia:UN: Watu zaidi ya bilioni 2 duniani hawapati maji salama ya kunywa

Kutokana na uhalifu huo, shirika la UNESCO limeutilia mkazo wito wake wa kuutaka umma na soko la sanaa katika biashara ya biadhaa za utamaduni kujiepusha kuingiza, kusafirisha, kununua au kumiliki bidhaa za kitamaduni kutoka Sudan.