Kashfa ya vichujia gesi
4 Novemba 2015Tuanzie na shirikisho la kabumbu la Ujerumani ambalo jana makao yake makuu yalivamiwa na vikosi vya polisi kusaka maelezo kuhusiana na tuhuma za udanganyifu.Gazeti la "Stuttgarter Nachrichten linaandika:"Vyombo vya sheria havikiandami kitu bila ya sababu.Eti kweli Euro milioni 6.7 zilikuwa fedha za hongo kutoka fuko la siri na ambazo waandalizi wa fainali za kombe la dunia wamedai kinyume na sheria warejeshewe na idara ya kodi za mapato kama gharama za maandalizi? Ikiwa jibu ni ndio,basi madai ya mchezo wa rushwa katika kuchaguliwa Ujerumani kuandaa fainali za kombe la dunia yatakuwa mabaya zaidi kuliko ilivyofikiriwa hapo awali.Ndio maana ni vyema kwamba vyombo vya uchunguzi vinazidisha shinikizo kutaka kujua yaliyotokea.
Kashfa ya vichujio vya gesi ya sumu
Kasheshe nyengine inaendelea kugonga vichwa vya habari nchini Ujerumani.Nayo ni ile kashfa ya udanganyifu ya kampuni mashuhuri ya magari ya Ujerumani Volks Wagen (FOLKS VAGEN).Gazeti la Braunschweiger Zeitung linaandika:"Misingi ya uwazi inabidi itangulizwe mbele kabisa hasa katika ukurasa huu mpya kuhusu tuhuma nyengine za idara ya usafi wa mazingira ya Marekani-EPA.Idara hiyo sio tu inaitia ila kampuni ya magari ya Volks Wagen,bali pia inazidisha makali ya tuhuma zake.Idara ya EPA inadai chombo kilichotiwa ndani ya magari ya VW,Audi na Porsche,kimebuniwa na kutengenezwa na tawi mashuhuri la Volks Wagen-Audi.Pindi tuhuma kutoka Marekani zikidhihirika ni za msingi,basi hapo,na Audi pia- kampuni jengine kubwa ya Ujerumani,itakuwa inagubikwa na kashfa ya kupunguza vipimo vya moshi wa sumu.Huo utakuwa pia ushahidi kwamba udanganyifu huo si kazi ya mtu mmoja,kama VW walivyokuwa wakidai hadi sasa.Na hilo litamaanisha pia kwamba udanganyifu umegeuka kuwa mfumo ndani ya kampuni ya VW.
Pegida wafurutu ada
Mada yetu ya mwisho magazetini inahusu kufurutu ada makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia -Pegida na mengineyo.Gazeti la Eisenacher Presse linaandika:"Katika ulimwengu mdogo wa Bachman,mbali na Maas na Goebbels,kuna waliokuwa pia wakimjua Karl-Eduard von Schnitzler.Kwasababu yeye ndie mchochezi,Bachman anamnyoshea kidole waziri wa sheria na vinne anajinyoshea mwenyewe.Ikiwa hilo tu ndilo Pegida wanalolijua,mtu anajiuliza,raia mstahiki aliyeingiwa na hofu anakwenda kutafuta nini katika utovu kama huo?
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse
Mhariri:Yusuf Saumu