Sierra Leone kuzindua kampeni ya chanjo dhidi ya Ebola
5 Desemba 2024Takribani wahudumu 20,000 wa afya watapatiwa chanjo hiyo. Haya ni kwa mujibu wa taarifa iliyotangaza kuanza kwa kampeni hiyo.
Taarifa hiyo pia imesema kuwa chanjo hizo kutoka Muungano wa Kimataifa wa Chanjo, Gavi zitatolewa kwa wahudumu hao wa afya wanaokabiliwa na hatari ya maambukizi kabla ya kuchunguzwa kwa mgonjwa, pamoja na madereva wa magari ya kubeba wagonjwa na waganga wa kienyeji na washauri, ambao mara nyingi huwa wa kwanza kuwasiliana na wagonjwa na jamaa zao.
Soma pia: Hatua za kuzingatia unapojihisi umeambukizwa Ebola
Taarifa hiyo imeongeza kuwa lengo ni kulinda vyema mfumo wa huduma za afya na wafanyakazi wake dhidi ya uwezekano wa mlipuko mwingine na pia kupunguza madhara ya virusi hivyo.
Waziri wa Afya Austin Demby ameitaja kampeni hiyo kama uwekezaji katika usalama wa watu wa nchi hiyo.