Siku nne za kuubadilisha ulimwengu
"Muktadha Mpya Ulimwenguni" ni kauli mbiu ya Kongamano la 45 la Kimataifa la Kibiashara la Davos linalofanyika Januari 21- 24. Miongoni mwa washiriki 2,500 watakokutana Uswis, kunakuwepo wakuu wa matafa zaidi ya 40.
Msimu wa tija
Wakati wa Kongamano la mwaka la Kiuchumi Duniani (WEF), Eneo dogo la Davos linajivunia uwepo watu wenye nguvu, matajiri na wenye ushawishi mkubwa. Wanajadiliana kwa upana masuala ya kimataifa kwa lengo la kuleta ustawi wa mataifa ulimwenguni. Vyombo vya habari vinataraiwa kuzingatia sana mkutano huo.
Suala la Uaminifu
Klaus Schwab, mwenye umri wa miaka 76 na mwasisi wa WEF analitazama kongamano hilo kama “jukwaa la ushirikiano kati ya sekta binafisi na umma.” Wakati dunia ikikabiliwa na vilio kadhaa, migogoro, matatizo ya kiuchumi, alisema ushirikiano “unahitajika zaidi kuliko awali.” Anasema WEF inaweza kutumika kama mwanzo wa kujenga imani ya ulimwengu”
Mambo muhimu ya kujadiliwa
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ni mmoja kati ya viongozi wakubwa duniani wanaohudhuria. Watendaji wakuu wa benki kubwa na makampuni mbalimbali vilevile wanakuwepo. Ajenda za mkutano huo zitaanzia katika suala la ugaidi, mabadiliko ya tabia nchi, buiashara ya kimataifa na fedha.
Ugaidi na migogoro
Mazungumzo kuhusu ugaidi yamepata umuhimu mpya kufuatia mashambilizi ya Ufaransa. Kundi la Dola la Kiislamu, vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria na machafuko katika matiafa ya kiarabu yamezusha hofu kubwa. Viongozi vilevile watajadili mgogoro wa Ukraine. Rais wa Ukraine Petro Poroshenko alikuwepo: Rais wa Urusi Vladimir Putin anahudhurii.
Mjadala wa mazingira
Mkutano wa kilele wa UN wa Mabadiliko ya Tabianchi wa mwishoni mwa 2015 una lengo la kufanikisha kupatikana kwa makubaliano ya pamoja ya kukabiliana na changamoto yake katika kipindi cha zaidi ya miaka 20. Makamo wa rais wa zamani wa Marekani Al Gore na Katibu Mkuu wa Umoja wa Matiafa kuhusu Tabia Nchi, Christina Figueres ni miongoni mwa wataoshiriki kujadili nafasi za makubalino hayo Davos
Makabiliano na Ebola
Mripuko wa Ebola katika mataifa ya Afrika Magharibi umeonesha umuhimu wa kukabiliana na kusambaa kwa virusi. Marais wa Guinea na Mali, mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni na wataalamu kadhaa watajadili kwa namna gani ugojwa huo unaweza kudhibitiwa.
Kurahisisha mzunguko wa fedha
Benki kuu nyingi za mataifa, watunga sera na mkuu wa shirika la fedha duniani watafanya ulinganifu wa fedha mjini Davos
Kushuka kwa bei ya mafuta
Kuporomoka kwa bei ya mafuta kunaeleza hali mbaya iliyopo katika mataifa yenye kuzalisha nishati hiyo, na kunapunguza faida itakonayo na mafuta hayo. Lakini kwa mataifa mengi, bei ya mafuta ghafi inafaida. Wadau mbalimbali wanahudhuria, wakiwemo wakuu wa makampuni kama ya magari ya General Motors, na makampuni ya mafuta na nishati pamoja na katibu mkuu wa OPEC.
Teknolojia na biashara
Kampuni ya Ujasiriamali ya Kichina ya Jack Ma’s, jukwaa la mauzo kupitia mtandao, Alibaba na mengine kwa pamoja watajadili kwa jinsi gani teknolojia inaweza kubadili hatma ya baadae kwa kutegea watoa uamuzi kutoka makampuni makubwa kama Microsoft, Yahoo, google na Facebook.
Wadau wote pamoja
Waandaaji wa kongamano hilo WEF hawakutaka taswira ya Davos igubikwe na watu wa tabaka la wasomi na mkutano wa mwaka wa matajiri. Masuala kama ya usawa wa mapato na kuongezeka kwa idadi ya wahamiaji ni miongoni mwa yatakayozingatiwa. Marais wa Benki ya Dunia na Shirika la Biashara Duniani, Mwasisi wa Microsoft Bill Gates, wataungana pamoja katika mjadala huo.
Davos eneo la biashara
Davos sio sehemu ya makubaliano ya kisiasa. Lakini makubalino ya biashara yatafaniyika katika mikutano mbalimbali. Mwekezaji mmoja katika sekta ya kibenki anasema. "Siku tatu za Davos zitanisadia kuepusha safari za miezi kadhaa"