1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aishi Manula apigwa na polisi baada ya mechi nchini Libya

16 Septemba 2024

Mlinda lango wa klabu ya Simba ya Tanzania Aishi Manula alipigwa na polisi baada ya kumalizika kwa mchezo mgumu wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF uliochezwa jana Jumapili nchini Libya.

https://p.dw.com/p/4keJC
African Cup of Nations | Elfenbeinküste, Abidjan | Alassane Ouattara Ebimpé Olympic Stadium
Picha: Braima Darame/DW

Afisa mmoja ambaye hakutaka kutambulishwa alisema aliona Manula akishambuliwa bila ya sababu yoyote na wachezaji wengine walirushiwa chupa na vitu vingine, hali iliyomtisha sana.

Afisa huyo aidha amesema, alishuhudia wachezaji wa Ahly wakiwashambulia waamuzi wa mechi hiyo na wasaidizi wao.

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili dhidi ya Al Ahly ulimalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Tripoli uliofurika mashabiki ambao muda wote walikuwa wakiwarushia wachezaji wa Simba chupa za plastiki.