1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSingapore

Singapore yamnyonga mwanamke baada ya miongo miwili

28 Julai 2023

Singapore imenyonga mwanamke mwenye umri wa miaka 45 aliyekamatwa na gramu 30 za dawa za kulevya aina ya heroine.

https://p.dw.com/p/4UV9R
Singapur | Protest gegen Todesstrafe
Picha: Roslan Rahman/AFP/Getty Images

Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya, CNB, imesema mwanamke huyo, Saridewi Binte Djamani alikutwa na hatia ya kumiliki karibu gramu 30 za heroine mwaka 2018.

Kunyongwa kwa Djamani kumefanyika licha ya maandamano ya kupinga kutekelezwa hukumu hiyo.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu, likiwemo Amnesty International yalikuwa yakizishikiza mamlaka nchini humo kumsamehe mwanamke huyo wakihoji kuwa adhabu ya kifo ni ukatili mkubwa.

Sheria za Singapore zinaruhusu adhabu ya kifo kwa walanguzi wa dawa za kulevya iwapo watakutwa na heroine ya zaidi ya uzani wa gramu 15.